Tunamshukuru Mungu kutujalia neema ya kuyafika maeneo mbalimbali ya nchi yetu kwa ajili ya semina . Semina hizi huandaliwa kwa kushirikiana na umoja wa makanisa au kanisa moja wapo mahali semina hufanyika.
Mara nyingi gharama za kuendesha semina hubebwa na huduma ya Mkate hai ministry isipokuwa ukumbi ambao huwa ni kanisa litakalo pendekezwa na umoja huo au kanisa litakalo shiriki pamoja nasi kuandaa semina.
Pamoja na kufanya semina,pia huduma imekuwa ikitoa watumishi kwenda kuhudumu ibaada za kawaida au kufundisha semina katika kanisa litakalo hitaji Huduma ya mafundisho au mahubiri, huduma hii hutolewa pasipo malipo yoyote.