Nov 30, 2016

Kusaidia wengine


Kama ilivyoandikwa katika Math.10:8 "mmepata bure, toeni bure ". Tunatoa bure vipawa, muda na fedha  zetu tulivyopewa kwa neema tuu na Mungu baba kuwasaidia wenye uhitaji. Tunafanya hivyo si kwa sababu tuna vingi sana hapana Bali ni kwa sababu ya pendo alilotupa Yesu mioyoni mwetu.

Tunajua kuwa tulicho nacho ni kidogo lakini twakusihi ukipokee hicho tunajua Mungu ataki ariki hata kiwe Cha baraka. Matendo ya Mitume 3:6 "...akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende ". Tunaomba upokee na kitunze kwa ajili ya wengine.

Tunakusihi ungana pamoja nasi Leo katika kuwasaidia wengine usisisema sina kitu toa hicho ulicho nacho kwani wako wanao kihitaji hicho kiwasaidie.Njoo umpe Mungu utukufu kwa kugusa maisha ya weingime, kwani ulizaliwa ili kusa abisha tabasamu katika nyuso za wanao kuzunguka.

Samuel

Author & Editor

Mimi si mchungaji au nabii bali ni mjumbe tu wa Mungu ambaye kwa neema yake amenitumwa kwa kizazi hiki niwaambie habari zake Mungu na falme wake,nami nakuombea Mungu akujalie neema ya kuelewa na kuyaweka katika matendo uliyo yasoma.