Dec 1, 2019

Aliye zaliwa mara ya pili aweza kutenda dhambi?.

Shalom kanisa.

Shalom kanisa.
Ndugu mmoja amekuja inbox na kumuliza swali la namna hiyo akiambatanisha na kifungia hiki

1 Yohana 5:18
Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.

Imenibidi nitazame maisha ya Wapendwa wetu walio tangulia kabla ya kujikita katika kifungu hiki.

Wa kwanza.
Tunasoma juu ya Safira na mkwe ambao walikuwa wamezaliwa mara ya pili ilikuwa hivi:

Matendo ya Mitume 5:1-3
Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali,
akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?

Pili.
Petro naye aliye kuwa mio goni mwa wanafunzi was Yesu alijiamini Sana kuwa hawezi kuanguka ktk mtego was Shetani wa kumkana Yesu. tunasoma

Sasa turudi kwa 1John 1:18.
1 Yohana 1:8-10
Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.

Angalia sentence hizi viuri ,Yohana anasema tukisema hatuna dhambi na sio hawana dhambi,tena twajidanganya na sio wanajidanganya, Tena  wala kweli haimo mwetu na sio haimo mwao, tena tukiziungama dhambi zetu na sio dhambi zao, tena hata atuondolee dhambi zetu sio awaondolee dambi zao, Tena  na kutusafisha na udhalimu wote sio kuwasafisha,tena  tukisema kwamba hatutendi dhambi na sio hawatendi dhambi,twamfanya yeye kuwa mwongo na sio wanafanya kuwa mwongo na Tena neno lake halimo mwetu na sio mwao. Hapa Yohana anasema na kanisa hasemi na wamataifa hapana na Tena hata yeye mwenyewe amejijumuisha humo . Naamini unaelewa vema kiswahili na unanielewa . Upo?.

1 Yohana 5:16-17
Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.

Anasema mtu akimwona ndugu sio mmataifa,hapa ndugu inamaanisha mwamini akitenda dhambi mtu aliyemwamini mwenzake aombe rehema kwa ajili ya yule atendaye dhambi na Mungu atamrehemu. Yohana anenda mbali kwa kutoa tafsiri ya dhambi kuwa Ni kila Jambo lisilo haki. Kwa hiyo tunapo fanya lolote lisilo haki kwa Mungu au kwa mtu yoyote yule hiyo ni dhambi hata kumjibu mtu vibaya katika comments hiyo ni dhakbi.

Kwa hiyo mstari huu wa 1Yohana 5 :18 no Ni lazima una ujumbe ndani yake ambao hatujaudlewa bado maana mwandishi hawezi kukipinga mwenyewe nasi twajua vema Biblia haijipingi yenyewe.

Kitabu hiki kinaelezea ukaribu zaidi wa Mungu na mtu ( fellowship) yeye Yohana hapa hazungumzii swala la kuhesabiwa haki Bali ushirika na Mungu ambao umejengwa katika kweli,anataka tumwelelze Mungu kweli yote kuhusu maisha yetu bila kuficha kitu kwa kuwa yeye Mungu anatuona kila tufanyalo Sasa Kama tunamficha kuwa hatukukosa kitu wakati yeye ameona tumkosea Hapo twamfanya kuwa yeye mwongo na kweli twajidanganya wenyewe maana kila kitu ameona .

Mpendwa wangu Kama kweli tunataka ushirika na Yesu ni budi tuwe wakweli mbele zake Hapo mtu awayeyote asikuzuie kumwambia Mungu umemkosa akusemehe yaani unahitaji toba kusudi akusafishe, acha kujaribiwa kuwa wewe umehesabiwa haki huna haja ya Toba, le kwa sababu ya kuhesabiwa haki basi hata tukijua tumekosea tuwe na kiburi Cha kuto omba msamaha kwa makosa yetu?.

Sikuhamasishi Utende dhambi  makusudi kwa kuwa utaomba Toba hasha maana maandiko yamekataa kabisa Jambo Kama Hilo tunasoma

Warumi 6:1-2
Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?
Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?

Sikia Mwana wa Mungu Biblia inasema kuwa maandiko Haipasi yafasiriwe kwa matakwa yetu Bali sisi yatupasa kufuata maandiko yasemacho na siyo kuyapotoa kukidhi matakwa yetu

2 Petro 1:20-21
Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Asante kwa kuwa. nami hapa. Naamini umepata kitu Cha kujifunza na ndugu uliye uliza swali naamini umepata jibu .

Kifupi Ni kuwa sote tunajaribiwa na tunaweza kuanguka. Wakati Petro anajitutumua kuwa hawezi kumsaliti Yesu,Yeau alimwambia Petro

Luka 22:31
Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano;

Atukuzwe Yesu  kwa kuwa anatuombea nyakati Zoe kusudi Imani yetu isitindike 

IKO TOFAUTI MOJA KATI YA ALIYEOKOKA NA ASIYEOKOKA. NAYO NI HII : MTU ASIYE OKOKA YEYE KUISHI KATIKA DHAMBI NI JAMBO LA KAWAIDA YEYE ANA AMANI KUISHI DHAMBINI Bali kwake aliye OKOKA HANA URAFIKI NA DHAMBI,MOYO WAKE HUUGUA SANA AKIMKOSA MUUMBA WAKE MPAKA AMEPATA MSAMAHA NDIPO AMANI HUJA


Samuel

Author & Editor

Mimi si mchungaji au nabii bali ni mjumbe tu wa Mungu ambaye kwa neema yake amenitumwa kwa kizazi hiki niwaambie habari zake Mungu na falme wake,nami nakuombea Mungu akujalie neema ya kuelewa na kuyaweka katika matendo uliyo yasoma.