Sala ya toba


Maamuzi bora na ya msingi kwa kila mmoja wetu tunayoweza kufanya ni maamuzi ya kuwa na uhusuano bora na sahihi na Mungu muubaji wetu. Hii ni kwa sababu mahusiano hayo hutupa nafasi ya kuwa na maisha bora si tu katika ulimwengu huu bali na ule ujao yaani ufalme wa Mungu.

Njia pekee ya kujenga uhusiano huu ni kwa kuokoka - yaani kumpokea Yesu Kristo ndani ya moyo wako kama Bwana na Mwokozi wako.

Ni imani yangu kuwa Roho Mtakatifu amekupa  fursa hii mikononi mwako  ili ufike mahali umgeukie Mungu wako kwa toba ya kweli na uokoke. Nimekuwekea sababu chache hapa chini kwa nini mhimu uokoke kama bado hujaokoka.

  • Kuokoka ni hatua ya awali ya kunakuepusha na hukumu inayo kuja ( Ebrania 2:3)
  • Kunakupa nafasi ya kutoka katika ufalme wa giza na kuingia ufalme wa Nuru.(Wakorosai1:13-14)
  • Unapewa uwezo wa kufanyika mtoto wa Mungu (John 1:12-13)

Hizo ni baadhi ya sababu na zipo nyingi.Hivyo ikiwa unataka kuokoka  basi nakusihi tafuta eneo tulivu, na omba sala hii kwa kuisoma ukimaanisha toka ndani ya moyo wako

Mungu baba wa Bwana wangu Yesu kristo . Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozitenda kwa kujua na zile niizokosa bila kujua maishani mwangu. Ninatubu kweli.Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu. Ninafungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho wako –uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na hata milele Ahsante kwa kunisamehe,na kuniokoa. Tangu leo Nimejitoa  kwako,nikutegemee na nikumikie  siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la YesuKristo. Amina".

Ikiwa umesema sala hii kwa dhati kabisa wewe umeokoa HONGERA. Nakushauri soma neno kila siku na sema na Mungu wako katika maombi Roho Mtakatigu yupo hapo kukusaidia. Tafuta kanisa la watu waliokoka uendelee kujifunza neno la Mungu.ikiwa utapenda kunijulisha juu ya muujiza huu wa wokovu usisite tuandikie nasi tutakutumia mafudisho katika email yako.