Mafundisho ya kibiblia
Dec 1, 2019
Masomo
Samuel
December 01, 2019
Shalom kanisa.
Shalom kanisa.
Shalom kanisa.
Ndugu mmoja amekuja inbox na kumuliza swali la namna hiyo akiambatanisha na kifungia hiki
1 Yohana 5:18
Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.
Imenibidi nitazame maisha ya Wapendwa wetu walio tangulia kabla ya kujikita katika kifungu hiki.
Wa kwanza.
Tunasoma juu ya Safira na mkwe ambao walikuwa wamezaliwa mara ya pili ilikuwa hivi:
Matendo ya Mitume 5:1-3
Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali,
akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?
Pili.
Petro naye aliye kuwa mio goni mwa wanafunzi was Yesu alijiamini Sana kuwa hawezi kuanguka ktk mtego was Shetani wa kumkana Yesu. tunasoma
Sasa turudi kwa 1John 1:18.
1 Yohana 1:8-10
Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.
Angalia sentence hizi viuri ,Yohana anasema tukisema hatuna dhambi na sio hawana dhambi,tena twajidanganya na sio wanajidanganya, Tena wala kweli haimo mwetu na sio haimo mwao, tena tukiziungama dhambi zetu na sio dhambi zao, tena hata atuondolee dhambi zetu sio awaondolee dambi zao, Tena na kutusafisha na udhalimu wote sio kuwasafisha,tena tukisema kwamba hatutendi dhambi na sio hawatendi dhambi,twamfanya yeye kuwa mwongo na sio wanafanya kuwa mwongo na Tena neno lake halimo mwetu na sio mwao. Hapa Yohana anasema na kanisa hasemi na wamataifa hapana na Tena hata yeye mwenyewe amejijumuisha humo . Naamini unaelewa vema kiswahili na unanielewa . Upo?.
1 Yohana 5:16-17
Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
Anasema mtu akimwona ndugu sio mmataifa,hapa ndugu inamaanisha mwamini akitenda dhambi mtu aliyemwamini mwenzake aombe rehema kwa ajili ya yule atendaye dhambi na Mungu atamrehemu. Yohana anenda mbali kwa kutoa tafsiri ya dhambi kuwa Ni kila Jambo lisilo haki. Kwa hiyo tunapo fanya lolote lisilo haki kwa Mungu au kwa mtu yoyote yule hiyo ni dhambi hata kumjibu mtu vibaya katika comments hiyo ni dhakbi.
Kwa hiyo mstari huu wa 1Yohana 5 :18 no Ni lazima una ujumbe ndani yake ambao hatujaudlewa bado maana mwandishi hawezi kukipinga mwenyewe nasi twajua vema Biblia haijipingi yenyewe.
Kitabu hiki kinaelezea ukaribu zaidi wa Mungu na mtu ( fellowship) yeye Yohana hapa hazungumzii swala la kuhesabiwa haki Bali ushirika na Mungu ambao umejengwa katika kweli,anataka tumwelelze Mungu kweli yote kuhusu maisha yetu bila kuficha kitu kwa kuwa yeye Mungu anatuona kila tufanyalo Sasa Kama tunamficha kuwa hatukukosa kitu wakati yeye ameona tumkosea Hapo twamfanya kuwa yeye mwongo na kweli twajidanganya wenyewe maana kila kitu ameona .
Mpendwa wangu Kama kweli tunataka ushirika na Yesu ni budi tuwe wakweli mbele zake Hapo mtu awayeyote asikuzuie kumwambia Mungu umemkosa akusemehe yaani unahitaji toba kusudi akusafishe, acha kujaribiwa kuwa wewe umehesabiwa haki huna haja ya Toba, le kwa sababu ya kuhesabiwa haki basi hata tukijua tumekosea tuwe na kiburi Cha kuto omba msamaha kwa makosa yetu?.
Sikuhamasishi Utende dhambi makusudi kwa kuwa utaomba Toba hasha maana maandiko yamekataa kabisa Jambo Kama Hilo tunasoma
Warumi 6:1-2
Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?
Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?
Sikia Mwana wa Mungu Biblia inasema kuwa maandiko Haipasi yafasiriwe kwa matakwa yetu Bali sisi yatupasa kufuata maandiko yasemacho na siyo kuyapotoa kukidhi matakwa yetu
2 Petro 1:20-21
Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Asante kwa kuwa. nami hapa. Naamini umepata kitu Cha kujifunza na ndugu uliye uliza swali naamini umepata jibu .
Kifupi Ni kuwa sote tunajaribiwa na tunaweza kuanguka. Wakati Petro anajitutumua kuwa hawezi kumsaliti Yesu,Yeau alimwambia Petro
Luka 22:31
Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano;
Atukuzwe Yesu kwa kuwa anatuombea nyakati Zoe kusudi Imani yetu isitindike
IKO TOFAUTI MOJA KATI YA ALIYEOKOKA NA ASIYEOKOKA. NAYO NI HII : MTU ASIYE OKOKA YEYE KUISHI KATIKA DHAMBI NI JAMBO LA KAWAIDA YEYE ANA AMANI KUISHI DHAMBINI Bali kwake aliye OKOKA HANA URAFIKI NA DHAMBI,MOYO WAKE HUUGUA SANA AKIMKOSA MUUMBA WAKE MPAKA AMEPATA MSAMAHA NDIPO AMANI HUJA
Nov 15, 2019
Maombi
Samuel
November 15, 2019
Shalom watu wa Mungu!
Leo naomba tuangalie kipengele kimojawapo mhimu Sana kwa kila aombaye kwa Mungu wa Bwana wetu Yeau kristo anaye tawala milele.
Kipengele hicho ni kusikia.Watu wengi hawana muda wa kutaka kusikia nakufuatilia kile wanaambiwa wakati wa Maombi,wengi wetu kazi yetu ni kuomba na tukisema ameni hatuna tena muda wa kutulia ili kupata malejesho ya kile tulikuwa tunaomba toka kwake tuliye mwomba.Jambo hili si la afya kwake aombaye kwa sababu.
Moja
Ili uweze kudumu katika Maombi unahitaji uwe na imani juu ya maombi., na kuligana Warumi 10:17[17]Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.Ni lazima uskie ndipo ujenge imani, Kama ni hivyo ni wazi kuwa katika Jambo lolote unalotaka kujenga Imani ni lazima usikia neno juu ya Jambo unalotaka kuwa na Imani nalo.Maombi yanahitaji usikie ili ujenge Imani juu ya Jambo unaloliomba au kulimbea,ndani ya Maombi ziko Imani tofauti tofauti kulingana na Maombi uyaombayao.Kuna Imani ya kukusubiri jibu la Maombi yako,iko Imani ya kuendelea kuomba wakati hauoni jibu likikujia mara moja, lakini pia kuna Imani ya kupokea jibu lako uliomba kwa Mungu.Haya yote yanahitaji usikiie . Biblia inatuambia kuwa ili tuwe na imani juu ya Mungu tunahitaji kuskia neno si la mtu flani bali Ni neno la Kristo. Warumi 10:17 [17]Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Tafusili ya kawaida ya maombi ni kuwa Maombi ni mawasiliano Kati ya mtu na Mungu wake. Katika maombi tunaongea na Mungu wetu naye hutujibu kama watototo wake,kwa kweli katika Maombi tuahojiana na Mungu wetu juu ya mambo mbalimbali yanahusu maisha yetu na pengine hata Yale yaliyo nje ya maisha yetu ya kawaida. Isaya 43:26 26]Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. Huwezi kuhojiana isipokuwa unasikia na unaelewa nini kinazungumzwa. Najua wengi hawaamini kuwa Mungu ansema na watu wake ,Hawa si kosa lao kuamini hivyo kwa kuwa bado hawajasikia akiongea nao na hata wakisikia hawezi kuelewa,kwao sauti hiyo huwa Kama kelele tuu.
Lakini niwakumbushe tu kuwa si rahisi kusikia na kuelewa lugha usiyo ijua kabisa vinginevyo utasikia sauti tuu ambazo huwa kama kelele tuu Mfano kwa mtu yule asiye jua lugha ya Mbwa hawezi kuelewa kitu akimwona mbwa wake anatikisa mkia lakini anaye elewa huwa anajua kuwa mbwa wake amefurahi.Pia kwa yule asiye kuwa na ufahamu juu ya Simba hawezi kuelewa kitu asikiapo sauti ya simba kwake huwa kelele tu bali walio na ufahau juu ya simba huwa wakisikia sauti ya simba huweza kuitambua kuwa Simba kwa mlio huu ana njaa au kwa mlio huu tayari kapata mawindo na ameshiba.
Nataka ujue kuwa kuto kujua kwako lugha ya watu au vitu flani hakumanishi kuwa watu au vitu Hivyo haviwasiliani hapana,unahitaji ujuzi husika ili uweze kusikia na kuelewa Mawasiliano , kadhalika unahitaji kujifunza jinsi Mungu asemavyo na watu wake.
Katika nyakati flani Samuel naye alipata wakati mgumu kuelewa kuwa ni Mungu anaongea naye kwa kuwa alikuwa haelewi Kama ni Mungu anasema japo alikuwa anasikia sauti.1 Samweli 3:3-10
[3]na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la BWANA, palipokuwa na sanduku la Mungu;
[4]basi, wakati huo BWANA akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa.
[5]Akamwendea Eli kwa haraka, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, Sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena.
[6]BWANA akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita, mwanangu; kalale tena.
[7]Basi Samweli alikuwa hamjui BWANA bado, na neno la BWANA lilikuwa bado halijafunuliwa kwake.
[8]BWANA akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akatambua ya kuwa BWANA ndiye aliyemwita yule mtoto.
[9]Kwa hivyo Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali pake.
[10]BWANA akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli akasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.Biblia inasema Samuel hakuekewa kwa kuwa alikuwa ni mtoto. Ni wazi kuwa Samuel alikuwa Hana ujuzi juu ya jinsi Mungu anavyoongsa na watu japo alikuwa anajua kuwa Mungu yupo na alimwamini.
Nakupa shauri Tafuta ujuzi unahusu kusikia sauti ya Mungu na kumwomba Roho Mtakatifu akusadie kusikia hakika utasikia Mungu akiongea nawe.
Saab ya pili.
Sababu nyingine ninayotaka ujue umhimu wa kusikia katika Maombi ni hii ya kuwa si kila mara uombapo utapewa kile umeomba moja kwa mjaa bali wakati mwingine unahitaji kufuata tarabu flani ili uweze kukipata kile uombacho kwa Mungu.Mfano mzuri juu ya hili ni huu wa mfalme Daudi tuusomao katika. 2 Samweli 21:1 [1]Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni. Like neno akautafuta uso wa Bwana ina maana kuwa Daudi aliingia katika Maombi ili kumsihi Mungu alete mvua juu ya nchi ,lakini unaona jibu la Mungu halikuwa kuleta mvua bali alimpa mfalme maelekezo nini kifanyike ili mvua inyeshe na tatizo la njaa litoweke juu ya nchi. Katika mistari inayofuata utaona kuwa Daudi aliposikia hayo alichukua hatua ya kuyatekeleza aliyo ambiwa na Mungugu. 2 Samweli 21:1-6,8-10
[1]Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.
[2]Ndipo mfalme akawaita Wagibeoni akawaambia; (basi Wagibeoni si wa wana wa Israeli, ila ni wa masalio ya Waamori; na wana wa Israeli walikuwa wamewaapia; lakini Sauli akatafuta kuwaua katika juhudi yake kwa ajili ya wana wa Israeli na Yuda;)
[3]basi Daudi akawaambia hao Wagibeoni, Niwatendee nini? Na kwa tendo gani nifanye upatanisho, mpate kuubariki urithi wa BWANA?
[4]Na hao Wagibeoni wakamwambia, Si jambo la fedha wala dhahabu lililo kati ya sisi na Sauli, au nyumba yake; wala si juu yetu kumwua mtu ye yote katika Israeli. Akasema Mtakayoyanena, ndiyo nitakayowatendea ninyi.
[5]Wakamwambia mfalme, Yule mtu aliyetupoteza, na kutufanyia shauri la kutuharibu, tusikae katika mipaka yo yote ya Israeli,
[6]basi, na tutolewe watu saba katika wanawe, nasi tutawatundika mbele za BWANA katika Gibeoni, katika mlima wa BWANA. Mfalme akasema, Nitawatoa.
[8]Ila mfalme akawatwaa hao wana wawili wa Rispa, binti Aya, aliomzalia Sauli, Armoni na Mefiboshethi; na wana watano wa Merabu binti Sauli, aliomzalia Adrieli, mwana wa Barzilai, Mmeholathi;
[9]akawatia mikononi mwa Wagibeoni, nao wakawatundika mlimani mbele za BWANA, nao wakaangamia wote saba pamoja; wakauawa siku za mavuno, za kwanza, mwanzo wa mavuno ya shayiri.
[10]Naye Rispa, binti Aya, akatwaa nguo ya magunia akajitandikia mwambani, tangu mwanzo wa mavuno hata waliponyeshewa mvua toka mbinguni; wala hakuacha ndege wa angani kukaa juu yao mchana, wala wanyama wa mwitu usiku.
Hebu fikiria Kama Daudi asingetega sikio lake kusikia na kuelewa kinachosemwa na Mungu wake.naamini tatizo lilie lingeendelea kumsumbua Daudi na Daudi angeendelea kuomba wakati hauoni jibu likikujia mara moja. Hata Sasa wapo watu wanendelea kuomba hawajaona majubu si kwa vile Mungu hajawajibu bali ni kwa sababu wamekosa usikivu kwani mahitaji yao yanahitaji wachukue hatua flani ili kupata waombalo.
Mfano mwingine ni huu wa mtume Paulo tuupatao katika kitabu cha 2 Wakorintho 12:8 [8]Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Mtume Paulo alikuwa anamwomba Mungu auondoe mwiba ulio kuwa unamsubua ubavuni pake alifanya Maombi Hayo zaidi ya Mara mbili mpaka tatu. Mungu akamjbu kuwa 2 Wakorintho 12:9 [9]Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
Ukitafakari jibu hili utagundua kuwa Paul aliomba mwiba uondoke lakini mwiba haukuondoka badala yake aliambiwa NEEMA YANGU YAKUTOSHA. Jibu hili ndilo lilibadili a mtazamo wa Paulo juu ya uwepo wa ule mwiba maana katika 2 Wakorintho 12:10[10]Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu. Mtazamo wake ulibadilika kabisa kwani pale mwanzo aliona mwiba ule kuwa kikwazo kwake vinginevyo asingeenda kuomba umtoke lakini badaye aliuona kuwa ni kitu Cha fahali na Cha kujivunia kwake.pia jibu hili lilimpa kujua kuwa ilikuwa ni kwa faida yake mwimba kuwepo aangalia 2 Wakorintho 12:7,10 [7]Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.[10]Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.
Sababu ya pili.
Sababu nyingine ya kwa nini Ni mhimu kutega sikio lako wakati wa Maombi hii ya kuwa……...
Kwa leo naomba nishie Hapa somo hili litaendelea, hapa usikose kuungaba nasi katika somo linalofuata
Ombi letu kwko Ni kuwa tuzidi kuombea kila wakati ili Neema ya kristo iwe pamoja nasi kila wakati tunapo andaa masomo haya kusudi tupate kusema kilicho Cha Mungu pekee. Nakutakia amani ya kristo katika kila Jambo ulifanyalo kwa utukufu wa Yesu Kristo.Ameni.
Nov 30, 2016
Why us
Samuel
November 30, 2016
Kama ilivyoandikwa katika Math.10:8 "mmepata bure, toeni bure ". Tunatoa bure vipawa, muda na fedha zetu tulivyopewa kwa neema tuu na Mungu baba kuwasaidia wenye uhitaji. Tunafanya hivyo si kwa sababu tuna vingi sana hapana Bali ni kwa sababu ya pendo alilotupa Yesu mioyoni mwetu.
Tunajua kuwa tulicho nacho ni kidogo lakini twakusihi ukipokee hicho tunajua Mungu ataki ariki hata kiwe Cha baraka. Matendo ya Mitume 3:6 "...akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende ". Tunaomba upokee na kitunze kwa ajili ya wengine.
Tunakusihi ungana pamoja nasi Leo katika kuwasaidia wengine usisisema sina kitu toa hicho ulicho nacho kwani wako wanao kihitaji hicho kiwasaidie.Njoo umpe Mungu utukufu kwa kugusa maisha ya weingime, kwani ulizaliwa ili kusa abisha tabasamu katika nyuso za wanao kuzunguka.
Subscribe to:
Posts (Atom)